Zimbabwe baada ya Mugabe: Taifa ambalo fedha za waliostaafu zinatoweka

0
23


Vesta (Kushota) na Teddy wakiwa nyumbani Zimbabwe.

Image caption

Vesta anasema kuwa anasikitika kuwa mume wake Teddie sanakaa mahali pamoja “asubuhi hadi jioni ”

Wanandoa Teddie na Vesta walidhani wataishi maisha mazuri yenye hadhi watakapostaafu.

Teddy mwenye umri wa miaka 85, na alifanya kazi ya usafi na kampuni moja kwa miaka 46 na baadae akapandishwa cheo kuwahudumia wageni katika kampuni hiyo.

Vesta anasema kuongezeka kwa mfumko wa bei umewapora fedha zao za kustaafu.

Mwaka mmoja uliopita thamani ya malipo ya uzeeni ya Bw. Teddie ilikuwa $80 (£66), lakini sasa ni dola 10.

“Nasikitika sana nikimuona mume wangu mpenzi akikaa mahali pamoja kuanzia asubuhi hadi jioni,” Vesta aliiambia BBC.

“Ningelipendelea kumpatia ndizi, chungwa ama kinywaji baridi. Lakini hatuna uwezo. Ndizi ni $0.40.”

Dalili za uchumi unaoporomoka inaonekana kila mahali. Katika maduka makubwa ya jumla ambayo yalikuwa na wateja wengi siku hizi yanapata wateja wachache sana na baadhi yao wanatafakari wanunue nini waache nini.

Bei ya bidha za kawaida kama sukari na mafuta ya kupikia imepanda kwa 200% katika kipindi cha miezi 12 hadi Juni, kwa mujibu wa takwimu rasmi. Sawa na gharama ya huduma ya afya.

Huku hayo yakijiri bei ya mkate imepanda karibu mara tano kutoka mwezi Aprili.

Kufikia mwezi wa Juni 2019, mfumko wa bei ulikuwa umegonga 98%. Mwezi Julai, sarafu ya dolla ya Zimbabwe ilizinduliwa baada ya miongo kadhaa ya kutumia dolla ya Marekani na sarafu zingine za kimataifa. Mfumko wa bei ya kila mwaka ilingezeka hadi 176%.

Thamani ya sarafu ya Zimbabwe imeendelea kushuka lakini serikali imepiga marufuku kuchapishwa kwa takwimu ya mfumko wa bei ikitaja madai ya kubadilishwa kwa sarafu ya nchi.

Mzozo wa hivi punde wa kiuchumi unakuja wakati ambapo rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anaadhimisha mwaka mmoja uongozini tangu alipochaguliwa kuongoza taifa hilo.

Robert Mugabe alitolewa madarakani baada ya mshirika wake wa karibu kumpindua kupita usaidizi wa wanajeshi mwezi Novemba mwaka 2017.

Uchaguzi uliandaliwa tarehe 30 mwezi Julai mwaka ulliofuata.

Rais Mnangagwa ametaja enzi yake ya utawala kama “Ukombozi wa pili” – akiangazia kufufua uchumi, kuimaraisha demokrasia na kubadilisha sera kali zilizowekwa na mtangulizi wake.

Awali Wazimbabwe walimuamini.

Huwezi kusikiliza tena

Kimbunga Idai: ‘Watu milioni 1.7 wapo katika njia kuu’ ya kimbunga Msumbiji na Zimbabwe

Walikuwa na matumaini baada ya kufanikiwa kumuondoa madarakani Bw. Mugabe ataweza kuwashawishi wawekezaji warejee nchini humo,ili kusaidia biashara zilizodorora lakini hayo hayakutimia

Kumekuwa na uhaba wa wa mafuta na serikali inasema haina sarafu za kigenu kuyanunua na kuanzisha mpango wa kutoa umeme kwa mgao.

Mamlaka pia inalaumu mitambo ya umeme iliyochakaa, mapato ya chi yanayotokana na huduma za umeme pamoja na ukame wa miaka 40 ambayo inatishia kusambaratisha mtambo mkubwa wa kuzalisha umeme katika eneo la Kariba.

Sauti za mara kwa mara za mitambo ya jenreta imekuwa jambo la kawaida mijini huku wafanyibiashara wa -nguo, hoteli, na maduka ya jumla wakijitahidi kundelea mbele na maisha licha ya bei yamafuta kuongezeka mara saba tangu mwezi Januari mwaka huu.

Hali hiyo imewafanya kuongeza bei ya bidhaa zaoili kukabiliana na athari za mfumko wa bei.

Hakuna suluhisho la haraka

Wawakilishi wa biashara wanasema kupotea kwa nguvu za umeme wakati mwingine kwa hadi saa 18 kwa siku, kumeifanya nchi kupoteza ushuru wa dola milioni 200 swa na (£165m).

Haki miliki ya picha
AFP

Waziri mpya wa kawi Fortune Chasi anaamni hakuna suluhisho la haraka la kukabiliana na changamoto hiyo

Licha gharama ya kuzalisha umeme hivi karibuni kupandishwa kwa 300%, huduma za umeme zinatolewa na serikali kwa bei ya chini zaidi. Zesa, ambalo ni shirika la kitaifa la umeme halina fedha kila wakati.

“Ghadabu ya wananchi inaelewekana na ipo haja kubuni njia mbadala ya kukabiliana na tatizo hili,” Bw. Chasi aliiambia BBC.

  • Mkoba uliojaa madola ya Mugabe waibiwa

“Tumekuwa tukiomba watu walipe bili zao za umeme kwa muda uliowekwa: Zesa linadai wateja wake dola bilioni 1.2.

“Watu kutoka kila sekta ya nchi wanadaiwa na Zesa.”

Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema mfumko wa bei utaandelea kushudiwa nchini humo.

Uzalishaji wa ndani bado uko chini hali inayosababisha utegemezi wa bidhaa kutoka nje wakati kuna uhaba wa sarafu za kigeni.

Gharama ya kundesha serikali inaendelea kuwa juu hali ambayo pia inawafanya waekezaji kutilia shaka ikiwa biashara zao zitakuwa salama.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais Mnangagwa, anayeonekana hapa akiwasha mwenge siku ya uhuru, anasema anataka kuimarisha hali ya demokrasia nchini Zimbabwe

Mamla nchini humo imebuni njia kadha za kubana matumizi- ikiwa ni pamoja na kupunguza fedha ilizokuwa inawalipia wananchi kupata mafuta, nguvu za umeme na huduma za afya ambazo zimepandisha juu bei za bidhaa.

Rais Mnangagwa anaamini hatua hizi ni muhimu kuimariasha uzalishaji wa ndani

“Haijakuwa rahisi- lakini najivunia hatua tuliyopiga kwa usaidizi wenu,” Rais alisema katika hotuba yake kwa taifa alipokuwa akitimiza mwaka mmoja madarakani tangu aliposhinda uchaguzi wa urais.

Athari ya kubana matumizi

Wakosoaji wa rais Mnangagwa wanasema amekuwa akitekeleza sera zinazoonekana kuwa kandamizi bila kushauriana na washika dau wengine nchini. Wanaamini kuwa anairejesha nyuma Zimbabwe miaka ya 2008.

Huo ulikuwa mwaka ambao Zimbabwe ilivunja rekodi na kuingia katika vitabu vya kihistoria.

Kiwango cha mfumko wa bei kilifikia 500bn%. Hati ya dhamana ya benki wakati huo ikiwa ni pamoja na ya trillion 100, zilitumika kununua bidhaa.

Mwanauchumi Godfrey Kanyenze anasema taifa hilo huenda linakodolewa macho na viwango vya juu zaidi vya mfumko wa bei.

“Mfumko wa kupitiliza wa bei hutokea wakati ambapo viwango vya mfumko wa bei vinapanda zaidi ya 50% kila mwezi,”anaelezea. “Mwezi Juni ilikuwa 39%.

Sasa tumesalia na 11% kufikia kiwango hicho cha mfumko wa bei wa kupitiliza, kwa hivyo hiki ni kiwango kibaya sana cha mfumko wa bei.”

Haamini serikali ya Zimbabwe inasuluhisho la muda mrefu la kukabiliana changamoto za kiuchumi zinazoikabili.

“Mataifa mengi yalioendelea yanafanya utafiti wa athari aza kiuchumi kabla ya kuanza utekelezaji wa sera mpya, Kwa mfano wanafanya utafiti wa kutathmini athari za kijamii na kujiandaa watakavyokabiliana na atahari hizo endapo zitajitokeza,” Anasema Kanyenze.

“Hapakuwa na matayarisho hayo, hasa katika masuala ya kulipa mishahara.”

Hatua moja ambayo imesaidia wananchi kukabiliana na ongezeko la mfumko wa bei ni kupunguzwa kwa gharama ya usafiri umma.

Hii inamaanisha kuwa wasafiri wanalipa robo ya pesa ambayo wanatozwa na wamiliki wa huduma ya uchukuzi wa kibinafsi kwa safari ile ile moja.

Wafuasi wa Bw. Mnangagwa wanahoji kuwa ni vigumu kutarajia kuwa mzozo huo wa kiuchumi utapata ufumbuzi wa haraka kwa sababu umekuwepo kwa miongo kadhaa.

Hata hivyo serikali inasema kuna matumaini mambo yatabadilika ikiashiria hatua yake ya hivi karibuni ambapo shirika la umeme lilipa Afrika Kusini deni la, Eskom, na kupata nafasi ya kuagiza kawi kutoka nje.

Huku hayo yakijiri serikali imeonya kuwa watu wajiandae kwa hali ngumu ya kiuchumi mwaka huu.

Hizi bilashaka sio habari njema kwa wananchi waliostaafu kama Teddie na Vesta lakini wanaishi kwa ”matumaini” siku moja mambo yatakuwa mazuri.Source link