Yaelezwa tiba mbadala kwa wagonjwa wa saratani ni hatari zaidi kuliko faida, Namna nyingine yaelezwa

0
11


Wagonjwa wa saratani wanapaswa kuwaambia madaktari wao kama wanatumia dawa za tiba asili kwa sababu baadhi ya dawa hizo zimetengenezwa na vitu vinavyoweza kusababisha kukoma kwa mchakato wa matibabu, mkutano wa wataalamu wa masuala ya maradhi ya saratani ulielezwa.

Vitunguu swaumu, tangawizi na vidonge vitokanavyo na majani ya ‘ginkgo’ kwa mfano, vinaweza kuchelewesha kupona kwa majeraha ya ngozi ikiwa saratani ya titi itasambaa.

Daktari wa upasuaji Profesa Maria Joao Cardoso, amesema hakukua na ushahidi kuwa tiba asili au krimu zilifanya kazi.

Kama kuna walakini, ni vyema kama dawa hizo hazitatumika, alieleza.

”Madaktari wanapaswa kufanya ziada katika kuuliza wagonjwa wao kuhusu dawa nyingine wanazozitumia wakati wanapopatiwa matibabu,” Profesa Cardoso alisema.

Alisema ilikuwa muhimu kwa wagonjwa kutazamwa na madaktari wao kabla ya kuanza tiba mbadala kwa saratani iliyosambaa kwenye ngozi.

Hali hii hujitokeza kwamtu mmoja kati ya watano wenye saratani ya matiti- na kwa kiasi kidogo kwa wagonjwa wenye saratani za aina nyingine.

DawaDawa zitokanazo na mimea na miti

Hatari ni kuwa bidhaa nyingi zinaweza kuingilia tiba za homoni au mionzi, na hizo huchelewesha mfumo wa damu kuganda- hali ambayo inaweza kusababisha vidonda kuchukua muda mrefu kupona.

Alidokeza baadhi ya bidhaa za dawa za asili kama mifano ambazo zinaweza kuchelewesha kuganda kwa damu:

  • ‘green chiretta’
  • ‘feverfew’
  • Vitunguu swaumu
  • ‘ginkgo’
  • mizizi ya ‘ginseng’
  • ‘hawthorn’
  • ‘horse chestnut’
  • Ukwaju

Haina madhara

Profesa Cardoso amesema haikushangaza kuwa wagonjwa na wanaowatunza kutafuta tiba za mitishamba au tiba mbadala ambazo pengine walihisi zingeleta matokeo tofauti.

Lakini amesema watu lazima wafahamu ”wanaweza kuleta madhara zaidi badala ya matokeo chanya”.

”Nia ya dawa ni muhimu kukumbuka ni: kutoleta madhara”, alisema.

BalungiTunda la balungi na maji ya matunda haya huathiri vimeng’enyo na kuharibu kazi ya dawa za saratani mwilini.

Katika tovuti yake, taasisi ya utafiti wa ugonjwa wa saratani imesema kuwa tiba mbadala inaweza kukomesha matibabu kufanya kazi.

Pia imesema ni muhimu kuepuka baadhi ya vyakula na vinywaji kama vile Balungi na machungwa wakati wa tiba, kwa kuwa vinaweza kuathiri tiba.

Grete Brauten-Smith kutoka taasisi inayoshughulikia wagonjwa wa saratani ya matiti nchini Uingereza amesema: ”Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa zilizothibitika mtandaoni na utafiti kuhusu bidhaa hizi, mjadala na wadau wa afya unaweza kumhakikishia mgonjwa kupata taarifa sahihi anazohitaji ili kufanya uchaguzi wanaoufahamu.”

Prof Cardoso amesema tiba kama za viungo mfano Yoga zinaweza kuwa na matokeo mazuri kwa mgonjwa katika kuyaboresha maisha yake.

Chanzo BBC

By Ally Juma.Source link