Watoto wa shule kunufaika na teknolojia mpya Burundi

0
15


Wanafunzi wakiwa mafunzoni BurundiHaki miliki ya picha
Bihub

Image caption

Wanafunzi wakiwa kwenye mafunzo ya teknolojia mpya

Bihub inasema kuwa Kampeni imewafikia watoto 13,000 katika wilaya tatu.

Natacha Nduwimana amekuwa akifundisha watoto lugha ya kompyuta kwa juma moja nchini Burundi, lakini ana matumaini kuwa kampeni yake itafanikiwa kuingia kwenye mtaala wa elimu.

Anasema matumaini yake ni kwa watoto wajifunze lugha ya kompyuta kwa kuwa ni muhimu kwa mustakabali wao.

  • Ni kwanini Tanzania inalaumiwa kwa ukandamizaji?
  • ‘Marubani watumia kamera iliyofichwa chooni kuwachungulia abiria’

Mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi wa taasisi ya Burundi Innovation Hub(Bihub) na wenzake wanajitolea kufundisha utengenezaji wa mifumo ya kutumia kompyuta kwa wanafunzi wa shule za msingi nchini Burundi.

Kampeni hiyo imelenga kuwafikia watoto 13,000 mjini Bujumbura, Gitega na Ngozi, juma lililopita waliwafikia watu 10,000, aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha
Bihub

Kampeni hiyo inashirikiana na shule ambazo zina vyumba vyenye kompyuta

”Tunatumia programu iitwayo Scratch ambayo huwawezesha watoto kutengenezaji wa vibonzo, michezo..baada ya saa moja mtoto anaweza kutengeneza michezo mwenyewe”.

  • Ni kwanini Tanzania inalaumiwa kwa ukandamizaji?
  • Jinsi Abu Bakr al-Baghdadi alivyouawa

”Tulikwenda kufundishalugha ya kompyutaeneo la Makebuko, ni eneo la nje ya wilaya ya Gitega, na tukawauliza watoto kuhusu kile wanachotaka kufanya watakapokuwa wakubwa. Baadhi walisema waalimu, mawaziri..Hawakujua kuhusu teknolojia mpya. Lakini baada ya siku chache wakiwa na sisi wengine walisema ‘ninapenda kuwa mtengeneza mifumo ya kutumia kompyuta’. kwa kuwa wamejifunza mambo mapya.”

Bi Nduwimana amesema kuwa changamoto aliyonayo ni ukosefu wa kompyuta kwenye shule na majumbani kwa ajili ya watoto kujifunzia.

Haki miliki ya picha
Bihub

Kundi hilo pia limewafundisha waalimu 200.

Ana matumaini kuwa programu itawavuta watoto kusoma masomo ya kompyuta katika masomo yao baadae.

”Hata kama watoto hawawezi kugharamia kuendelea na mazoezi,lakini watakapofika elimu ya sekondari na chuo kikuu wanaweza kuchagua kujifunza masomo hayo kwa kuwa wana elimu ya awali kuhusu somo hilo”.Source link