Uwanja wa ndege wafunguliwa tena, kiongozi aonya Hong Kong huwenda ikatumbukia shimoni

0
36


Baada ya maandamano hapo jana uwanja wa ndege wa Hong Kong umeruhusu tena safari za ndege. Kiongozi wa kisiwa hicho Carrie Lam ameonya kuwa Hong Kong inaweza kutumbukia shimoni ambako itakuwa vigumu kujitoa.

Hongkong Proteste gegen China PK Carrie Lam (Reuters/T. Peter)

Shughuli kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong ambao ni miongoni mwa viwanja vinavyohudumia wasafiri wengi zidi duniani, zimeanza tena taratibu asubuhi ya leo, lakini mamlaka ya uwanja huo imeonya kuwa baadhi ya safari zinaweza kuendelea kutatizwa. Tangazo la kurejesha safari za ndege limewekwa kwenye huduma ya simu za mkononi, au app ya uwanja huo mnamo saa kumi na mbili asubuhi saa ya Hong Kong.

Uwanja huo ulikuwa umeahirisha safari zote za ndege jana Jumatatu, baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika katika ukumbi wanakofikia wasafiri. Wengi wa waandamanaji hao wameondoka usiku wa kuamkia leo, wakibaki wapatao 50 tu.

Soma zaidi: Yanayojiri Hong Kong: Maalfu ya watu waendelea kuandamana

Hongkong Proteste gegen China - Generalstreik Flughafen (picture-allaince/AP/Royston Chan)Safari zote za ndege ziliahirishwa jana katika Uwanja wa Hong Kong

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa wasafiri wapatao 100 walikuwa wamepiga msitari kwenye ofisi ya shirika la ndege la Cathay Pacific asubuhi ya leo. Shirika hilo rasmi la Hong Kong limetishia kuwafukuza wafanyakazi wake watakaobainika kuunga mkono waandamanaji.

Onyo kuhusu athari mbaya kwa Hong Kong

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Wakati hayo yakijiri, kiongozi wa Hong Kong anazongwa na shinikizo, Bi Carrie Lam ametetea mienendo ya polisi katika kukabiliana na mandamano, ingawa miongoni mwa malalamiko ya waandamanaji hao ni jinsi polisi wanavyotumia nguvu za ziada kukandamiza vuguvugu lao. Lam pia ametoa mwito kwa kila mmoja kujizuia kufanya fujo.

”Hebu tumia dakika moja kufikiria jiji letu. Mnataka kulitumbukiza shimoni na kulivunja vipande vipande? Tunahotakiwa kufanya hivi sasa ni kujiepusha na ghasia na kuheshimu sheria,” amesema Lam na kuongeza kuwa baada ya kurejeshwa kwa hali ya utulivu, ndipo ”tunapoweza kuanza mjadala wa kumaliza mgawanyiko katika jamii.”

Soma zaidi: Hong Kong yaufuta muswada tata wa sheria

Vyombo vya habari nchini China leo hii vimeyakosoa vikali maandamano ya jana, vikiwataja wanaharakati wa demokrasia kama magenge ya wahuni, ambayo matakwa yake hayawezi kuridhiwa kamwe. Vimegusia pia pia uwezekano wa vikosi vya China Bara kuingilia kati kuyavunja maandamano hayo.

Chipuko la ugaidi?

Hong Kong Protest (picture-alliance/ZUMAPRESS.com/M. Candela)Waandamanaji wanaripotiwa kurejea tena leo katika uwanja huo kuendeleza vuguvugu lao

Mamlaka ya China pia imeyakemeya vibaya maandamano hayo, ikisema yanaashiria kuchipuka kwa ugaidi. Gazeti la mrengo wa kizalendo la The Global Times limesema waandamanaji wenye misimamo mikali wametumia fujo dhidi ya polisi, wakitumia silaha za hatari.

Taarifa za hivi punde zimeeleza kuwa mamia ya waandamanaji walikuwa wakirejea katika uwanja wa ndege kuendeleza waliyoanza jana, wakivalia fulana nyeusi ambazo zimekuwa nembo yao.

Vuguvugu hili la maandamano lilianza kwa nia ya kupinga sheria ambayo ingewezesha washukiwa wa uhalifu kisiwani Hong Kong kupelekwa katika mahakama za China Bara. Muswada wa sheria hiyo umesitishwa, lakini haujafutwa kabisa.Source link