Ubunifu wa mavazi ya uyoga na mananasi unaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

0
6


Handbag made of mycelium

Haki miliki ya picha
Bolt Threads

Image caption

Mkoba uliotengenezwa na uyoga

Vijana wengi wanapenda kununua nguo kila mara ili kuendana na mitindo iliyopo kwa wakati huo.

Mara nyingine watu maarufu huwa wanatoa msukumo mkubwa kwa watu kufanya uchaguzi wa mavazi aina fulani.

Soko la mavazi kidigitali pia umeongeza uhitaji wa nguo kukua kwa kasi na hivyo kuathiri soko la mitindo linaathiri maendeleo endelevu.

Nchini Uingereza, wateja huwa wananunua nguo mara mbili kwa kwingi kama miongo iliyopita.Kama ilivyo nchi nyingine za ulaya.

  • Mlemavu asiyeona kubuni mavazi ya stara
  • Kwa nini Instagram inawagharimu zaidi maharusi?

Nguo ni asilimia 20 ya taka zilizopo duniani na kusabisha gesi ukaa kwa asilimia 10.

Wanaharakati wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi wameandana na kuwataka watu kuacha kununua nguo mpya ili kupinga fashioni.

Imekuwa adhabu

Jambo hili linawezekana kweli kwa mtu anayependa mitindo , kupunguza matumizi yake ya kununua nguo ili kuhifadhi mazingira.

Namna mpya ya kutengeneza nguo inaweza kukabiliana na tatizo hili na kuchukua mbadala wa nguo zinazotengenezwa na pamba na ngozi.

Wakati ngozi ni bidhaa inayotokana na nyama, kutengeneza bidhaa hiyo huwa inatumia kiasi kikubwa cha maji na kutumia kemikali ambazo sio rafiki huwa zinatumika kutengenezea.

  • Uyoga wachangia kutunza msitu wa Nou

Suluhisho sahihi la kuacha matumizi ya ngozi ni kutumia majani ya mananasi , kama vile kampuni maarufu za mikoba kama Hugo Boss na H&M huwa wanatumia.

Nmana nyingine ya kupunguza matumizi ya ngozi ni kutumia uyoga, Uyoga ambao umekuwa ukitumika kama chakula unaweza kutengeneza nguo pia.

Uyoga unastawi kwa wingi na hauhitaji uangalizi sana na unaweza kuota ndani ya siku chache..

Wateja wengi wamevutiwa na bidhaa hizo ambazo zinaunga mkono kampeni ya maendeleo endelevu, ingawa changamoto bado ni gharama kuwa juu zaidi.

Vumbuzi nyingi zinakutana na changamoto kubwa ya gharama ambapo inawafanya watumiaji wanashindwa kununua .

Mara nyingine bidhaa hizo zinakuwa zina gharama sawa na ngozi.

Mbadala wa Pamba

Kama ilivyo ngozi, pamba pia ni rasilimali muhimu katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Nguo moja aina ‘jeans’ inatumia lita 15,000 za maji.

Asilimia 40 ya nguo zinazovaliwa duniani zinatengenezwa na pamba.

Mbadala wake ni nguo amazo zinatengenezwa kwa nyuzi na utengenezaji wake unahitaji asilimia 95 ya maji kiwango ambacho kiko chini na utengenezaji wa pamba.

Nguo zinazotengenezwa na miti zinafanana kabisa na nguo iliyotengezwa na pamba.

Utengenezaji wa nguo kwa kutumia pamba bado ni nafuu tofauti ingawa kuna umuhimu wa watu kuzingatia maendeleo endelevu ili kukabiliana na changamoto ya mazingira.

Nunua bidhaa nzuri kwa kiasi

Kuna uhitaji wa watu kuzingatia namna wanavyonunua bidhaa zao, ni vyema kununua bidhaa kiasi ambazo zina ubora mzuri.

” Unaweza kununua nguo 30 na zikakutosha , bila kuathiri mazingira , amesema mtaalamu wa mavazi Dkt. Blackburn.

Miaka ya hivi karibuni wateja wa nguo pia wameanza kuelewa kuwa kununua nguo za gharama nafuu si jambo jema hata kama matangazo huwa yanavutia lakini athari ni kubwa kwa muda mfupi.

Haki miliki ya picha
Piñatex

Image caption

Nyuzi zinazotoka na majani ya nanasi yanaweza kutengeneza nguo

Watu sasa wameanza kuwa na ueleo zaidi wa mazingira na gharama inatumika kutunza mazingira, watu wameanza kununua nguo ambazo haziishii kutupwa .

Wataalamu wanakiri kuwa ni vigumu kufikia lengo kwa wakati kwa sababu watu wanahitaji kuzoea mabadiliko hayo.Source link