Trump na Kim Jong Un kuzungumza leo, Hanoi

0
46


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Vietnam, kuelekea mkutano wao wa pili na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Ndege ya Rais wa Marekani Air Force One ilitua katika uwanja wa Ndege wa Hanoi, Noi Bai saa kadhaa baada ya Kim Jong Un, kuwasili katika mji mkuu wa Vietnam kwa Gari.

Mkutano kati yao utafanyika leo na kesho, baada ya mazungumzo yao ya kwanza yaliyofanyika Singapore mwaka uliopita.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumzia hatua iliyopigwa juu ya kuiweka huru rasi ya Korea na silaha za nyuklia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mji wa Hanoi, mwenyeji wa mkutano huo

Kulikuwa na ulinzi mkali mjini Hanoi, wakati kiongozi wa Korea kaskazini alipowasili mjini humo na kupokelewa na umati wa watu waliokuwa wakipungia bendera, akitokea mji wa mpakani wa Dong Dang kwa gari.

Katika safari yake hiyo Kim Jong Un anadhaniwa kuwa amesafiri na dada yake Kim Yo-jong na mmoja wa Wapatanishi wake muhimu Jenerali wa zamani Kim Yong- chol.

Wakati msafara wake huo wa Treni ukipita nchini China, kutoka Korea Kaskazini, barabara zilifungwa na vituo vya Treni kufungwa.

Tofauti na mwenziye wa Korea, Rais Trump alisafiri mjini Hanoi kwa ndege. Na kuwasili mjini humo jana jioni.

Kwa mujibu wa ratiba yao, Rais Trump atakutana na Kim Jong Un kwa mazungumzo mafupi baina yao leo Jumatano jioni, na baadaye watakuwa na chakula cha pamoja na washauri wao. Huku siku ya Alhamisi wakiendelea na mazungumzo yao.Source link