Sudan: Ramadhan inavyowapa motisha waandamanaji kushinikiza mageuzi

0
77


Sudanese men sit together as they are served Iftar at sunset during the Muslim holy month of Ramadan, at their protest outside the army headquarters in Sudan - 10 May 2019Haki miliki ya picha
AFP

Zaidi ya mwezi mmoja baada ya majeshi nchini Sudan kuondoa madarakani utawala wa Omar al-Bashir, umati mkubwa watu umeendelea kupiga kambi usiku na mchana mbele ya makao makuu ya kijeshi katika mji mkuu wa Khartoum.

Wanahisi kuwa utawala wa mpito unaoongozwa na baraza la jeshi hautaki kuhamisha madaraka kwa utawala wa kirai.

Wamejitolea kufanya hivyo licha ya kuwa wanaendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Nguvu ya uwepo wao katika eneo hilo inadhihirika wakati wanapokuja pamoja kufungua mfungo wao (Iftar) jua linapotua.

Punde baada ya wao kusali na kula waandamanaji wanaanza kuimba kwa pamoja: “Utawala wa kirai ama mageuzi ya daima.”

Wengine wanajibu kwa mkufuatilia na maneno haya : “Sitarudi nyuma, Nina mahitaji.”

Maelfu ya watu huanza kufika- wengine wakiwa wamebeba vyakula vyao wenyewe pamoja na maji kutoka nyumbani na wengine huamua kupika pamoja katika eneo lililotengewa waandamanaji.

  • Bashir ashtakiwa kwa vifo vya waandamanaji

Vyakula pia hutolewa na wanawake ambao wanawaalika watu waliyojitolea kuunga mkono mkono maadamano hayo kupitia mitandao ya kijamii kwenda majumbani mwao kuchukua vyakula hivyo.

Kampuni nyingi pia zimejitolea kuwapelekea maji ya chupana vyakula kwa kutumia magari makubwa ili kuhakikisha hakuna mtu anaeshiriki maandamano hayo anaumia kwa njaa au kiu wakati huu wa mfungo wa ramadhan.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Waandamanaji wanahofia maafisa wa utawala uliyopita wanaweza kurejea madarakani

Wakati wa kutoa hotuba ukifika wanaharakati na watu wa kawaidi ambao hawakuwahi kufikiria kuzungumza hadharani wanapata furasi ya kuhutubia umati wa watu.

Wanazungumzia mateso yanayodaiwa kutekelezwa na majeshi na wanamgambo waliyokuwa karibu na utawala wa Omar al Bashiri uliyong’olewa madarakani – na jinsi familia zao zilivyoathiriwa.

  • Onyo la mvua kubwa latolewa Tanzania

Wanaelezea vitu ambavyo watu wengi hawajawahi kuvisikia.

Wengi wa wzungumzaji wanatoka katika maeneo yaliyoathiriwa na ghasia kama vile Darfur ama Kordofan kusini.

Baadhi yao wanaelezea jinsi wamekua waathikiwa wa ujenzi wa bwawa ambao walitolewa makwao kwa lazima.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Sanaa ya uchoraji ni moja ya vitu vilivyopata umaarufu mkubwa katika maandamano ya Sudan

Familia za waandamanaji walouawa wakati wa mandamano pia zinapewa nafasi ya kuzungumza.

Watu wanazungumza usiku kucha na kuhamasishana jinsi maandamano hayo yatakua na manufaa siku zijazo.

Hatua hiyo imefanya watu wengi zaidi kujitokeza usiku katika eneo lililotengewa wandamanaji na wengine wameamua kukaa katika maeneo ya wazi kama vile maduka ya kahawa au kulala nje kwenye manyasi karibu na njia ya reli.

Joto kali

Ni waandamanaji wachache wanaokaa nje nyakati za mchana kutokana na viwango vya juu vya joto mjini Khartoum.

Japo kuna baadhi ya watu ambao wamejitolea kuwapatia waandamanaji vitu kama feni tamba na mitambo ya kusaidia kupungoza joto bado hawajafanikiwa kupunguza makali ya joto hilo kwa sababu viwango vya joto hupanda kwa zaidi ya nyuzi joto 40.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Baadhi ya waandamanaji wanawapikia wenzao katika eneo lililotengewa maandamano hayo

Lakini joto hilo kali halija wazuilia wachoraji kuendelea na sanaa yao ya kupaka rangi kuta za mijengo iliyokaribu na eneo wanalopiga kambi nyakati za mchana.

Katika maeneo menginE mjini Khartoum, foleni za watu wanaotoa pesakatika mitambo ya ATM zinaonekana,vituo vya mafuta vinafanya kazi na katika maduka ya kuoka mikata pia yamerejelea shughuli zao.

Tangazo la kupanda kwa bei ya bidhaa hizo ilichangia kuzuka maandamano, yaliogeuka kuwa shinikizo la kumtaka rais Omar al- Bashir kuondoka madarakani.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Watu wanalazimika kupanga foleni kapata pesa mjini Khartoum

Licha hali hizo watu katika mji huo wana furaha na matumaini kuwa mambo yatabadilika.

Wanawake pia wanajisikia huru zaidi, na wanaume wamekuwa wakiwashinikiza kujitolea kushirika maandamano yanayoendelea kwa kutumia maneno “Kandaka”, wakimuashiria malikia wa ufalme wa Kush uliyoongoza Sudan kwa maelfu ya miaka iliyopita.

Huwezi kusikiliza tena

Picha hii inaashiria nafasi ya wanawake katika maandamano dhidi ya serikalai ya Sudan.

Kabla ya Bw. Bashir kuondolewa madarakani neno ”Kandaka” lilikua halitumiwa na waandamanaji wa kike.

Lakini ni jina ‘thawra’ alilopewa Alaa Salah, mwanafunzi wa miaka 22 aliyekuwa sura ya maandamano ya kupinga utawala wa Bashir baada ya kanda ya video yake akiongoza maandamano hayo kusambaa katika mitando ya kijamii.

Hatua zilizopigwa kupitia maandamano hayo ni ishara kuwa mageuzi ni yanashuhudiwa nchini Sudan – na waandamanaji wanataka kuhakikisha mabadiliko mengine yatakayopatikana yalinde maslahi yao.Source link