Spika wa bunge Job Ndugai amesitisha uwakilishi wa mbunge Stephen Masele, katika Bunge la Afrika hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili (+Video)

0
57


Spika Job Ndugai ametangaza kusitisha uwakilishi wa Mbunge Stephen Masele kwenye Bunge la Afrika (PAP) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge hilo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu mpaka atakapohojiwa na Kamati ya maadili ya Bunge.Spika amesema Masele ana matatizo ya kinidhamu na amekuwa akifanya mambo ya ‘hovyo hovyo’ ikiwemo kugonganisha mihimili.

“Stephen Masele ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyohovyo, ndiyo maana tumemuita atufafanulie huenda yuko sahihi, lakini anafanya mambo ambayo ni hatari kubwa, amekuwa akichonganisha mihimili miwili, ni amejisahau sana, amekuwa akichonganisha mihimili ya Serikali tena ya juu kabisa.” amesema Ndugai.

By Ally Juma.Source link