Raia kadhaa wa kigeni ‘wakamatwa’ na dhabu feki Kenya

0
63


DhahabuHaki miliki ya picha
AFP/GETTY IMAGES

Raia wawili wa Tanzania ni miongoni mwa washukiwa kadhaa waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya kuuza dhahabu feki nchini Kenya.

Washukiwa hao walikamatwa mamilioni ya dola na dhahabu feki kufuatia msako mkali unaofanywa nchini humo kuwasaka wafanyibishara huyo haramu.

Wengine waliokamatwa ni pamoja Mnigeria na Mcongo mmoja pamoja na wenyeji wao wanne ambao ni raia wa Kenya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Siro amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema kuwa jeshi hilo halina taarifa zozote kuhusu raia hao wa waliyokamatwa Kenya.

Katika kisa cha hivi karibuni mmoja wa wafanyabiashara alidaiwa kufanya jaribio la kumtapeli mwana wa Mfalme wa Dubai kwa kumuuzia dhahabu feki lakini alikamatwa na polisi kbala ya kutekeleza uhalifu huo katika duka moja lilipo mtaa wa Lavington nje kidogo ya mji wa Nairobi.

Hatua hiyo inasemekana ilimfanya Rais Uhuru Kenyatta aliagiza msako mkali kufanywa baada ya kupata malalamiko dhidi wafanyibiashara hao.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya Jumatatu iliyopita kikosi cha polisi wa dharura kilivamia nyumba moja eneo Kileleshwa jijini Nairobi na kukamata dhahabu feki na magari manane na washukiwa wanane.

Vitu vingine pia vilikamatwa katika nyumba hiyo iliyokuwa ikilindwa na maofisa wa usalama.

Mkuu wa idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) George Kinoti alizishauri balozi zote nchini humo kuwatahadharisha wananchi wao kuhusu jambo hilo.

Tahadhari hii imetolewa ili kuzuia uhalifu kutokana na kesi zinazohusisha ununuzi na uuzaji wa dhahabu nchini.” ilisema taarifa yake.

Mshukiwa wa hivi punde kukamatwa kwa msako dhidi ya dhahabu fiki ni mfafibiashara maarufu jijini Nairobi Jared Otieno.

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, mabilioni ya fedha gushi yamekamatwa katika maeneo tofauti ya jiji la Nairobi.

Mwezi Februari, polisi walisema walikamata pesa bandia sawa na shilingi bilioni 32 katika nyumba moja maeneo ya Ruiru, Kiambu viungaji mwa jiji la Nairobi na mwezi Machi walikamata shilingi bilioni 2 zilizokuwa feki katika tawi la benki ya Barclays zilizokuwa zimewekwa kwenye boksi lililotengwa kwa ajili ya pesa zilizowekwa na wateja: Kenya: Polisi waivamia benki kwa msako wa pesa bandia

Lakini mmiliki wa pesa hizo , Bwana Eric Adede, alikanusha kuwa pesa hizo zilikuwa bandia na akaiomba benki iwaaamuru polisi kuleta pesa hizo mahakamani.Source link