Ni kwanini wavulana hawa walitembea kwa miguu maili 150?

0
13


Guy na Nelson,Haki miliki ya picha
JACK LOSH

Image caption

Guy na Nelson,

Watoto waliotembea na kuingia katika kijiji kimoja kilichopo kaskazini-mashariki mwa Jamuhuri ya Afrika ya kati mapema mwaka huu , baada ya kutembea mwendo mrefu wakipitia msitu na nyika za savana , ni ishara ya tatizo linaloendela kukua : baada ya miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe , maelfu ya watoto nchini humo wamekuwa yatima. Je kuajiri idadi kubwa ya wazai wa kuwalea linaweza kuwa suluhu?

Siku moja asubuhi katika kipindi cha msimu wa majira ya kiangazi Henriette Idjara alikuwa akisafiri kuelekea jijini kwao nyumbani alipowaona wavulana wadogo wawili wakitembea kando ya mto. Nguo zao zilikuwa zimechanika huku zikiwa zimejaa matope na vumbi. Wavulana hao walikuwa wanaonekana kama waliopotea wakihitaji msaada.

Henriette hakuweza kuwapuuza. Kama mama mwenye umri wa miaka 53 ambaye aliwapoteza watoto watano wake mwenyewe, alihisi huruma ya mzazi ikimwamwia atoe usaidizi.

“Mnafanya nini hapa?” aliwauliza.

Miaka hao wawili, Guy na Nelson, walimwambia kuwa askari wa waasi walikuwa wamevamia kijiji chao na kumuua kikatil baba yao, miezi kadhaa iliyopita. Mama yao alikuwa metoroka zamani. Baada ya kuishi maisha ya hofu ya mahsmbulio zaidi na kushindwa kupata chakula, hatimae wavulana hao waliamua kuondoka kwa miguu yao kutafuta kazi.

Image caption

Ghasia hazikoma katika Jamuhuri ya Afrika ya kati licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwezi Februari

Wakati Henriette alipowapata, wiki moja kabla walikuwa wametembea takriban maili 150.

“Walikuwa wanajaribu kufika kwenye mgodi wa dhahabu ,” anasema Henriette. “niliwaambia, sikieni, mahali pale ni hatari. Kuna ghasia nyingi huko.'” Badala yake aliwapeleka nyumbani kwake.

Uliwakuwa ni wakati ambao yeye na mume wake , Jean-Philippe, walikuwa wakiusujbiri. Wana mvulana mmoja na wasichana watatu , lakini watoto wao wengine watano walikufa kutokana na magonjwa ya malaria, uti wa mgongo na magonjwa mengine. Kutokana na vifo hivyo waliamua kujisajiri kama wazazi wa kueleana walikuwa wakisubiri kupewa watoto.

“Huu ni wito wetu ,” anasema Jean-Philippe, ambaye ni mwalimu wa mafunzo ya dini kanisani . “watoto wote wanapaswa kutunzwa, kwasababu wanaweza kukua na kujenga jamii bora kuliko ile tuliyonayo sasa .”

Jamuhuri ya Afrika ya kati ilidumbukia katika limbo la ghasia mwaka 2013 wakati waasi wa kiislamu wa kundi la Seleka waliponyakua mamlaka, jambo lililochochea uundwaji wa kundi la wanamgambo wa kikristo la “anti-balaka”.

  1. Myanmar inachunguza ‘utumwa wa watoto’
  2. Watoto ‘wanaozuia mvua kunyesha’

Maelfu ya watu walisambaratika katika ghasia hizo zilizofuatiwa na ongezeko kubwa la watoto yatima au watoto waliotengana na wazazi wao. Mashambulio ya ghasia yamekuwa yakiendela kote nchini humo tangu wakati huo .

Mkataba wa amani uliosainiwa mwezi Februari umeleta matumaini ya usitishwaji wa kudumu wa mzozo, lakini bado haujaweza kuwa suluhisho la amani na utulivu nchini humo. Wavulana Guy na Nelson walianza safari yao ya miguu wiki kadhaa baada ya kusainiwa.

Henriette na Jean-Philippe waligundua moja ya matukio mabaya zaidi waliyokabiliana nayo baada ya kukutana nao kwenye ukingo wa mto.

Kwa mujibu wa wavulana hao , wanamgambo waliokuwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK47 walivamia kijiji chao kwa pikipiki, na kuanza kuwapiga risasi raia bila kubaguana kuchoma nyumba zo moto. Baadhi ya wakazi walitorokea misituni, lakini baba yao alibaki kuilinda nyumba yao . Aliwapiga risasi washambulia kwa mshale, lakini hatimae alikamatwa na kukatwakatwa na upanga hadi kufa.

Guy na Nelson waliweza kuwatoroka wauaji baada ya kukimbilia msituni na kujificha huko . “tushuhudia kila kitu ,” anasema Guy, ambaye ni mdogo kwa Nelson.

Baada ya hapo , wakati mmoja wanamgambo walikuwa wamewafukuza wakakikimbia kijiji ambacho kilibaki hakina watu, ndipo walipotoka mafichoni na kuweza kuuzika mwili wa baba yao ambao ulikuwa umeharibika.

Tangu walipowachukua wavulana hao na kuwalea, Henriette na Jean-Philippe walimeweza kuwapatia upendo na nidhamu na kuwafanya wawe kama watoto wa kawaida.

Haki miliki ya picha
JACK LOSH

Image caption

Guy na Nelson wakiwa pamoja na Henriette na Jean-Philippe

“Tunawasaidia kila tuwezavyo ,” anasema Henriette.

“Tunawaambia kuwa hawapaswi kufikiria sana kuhusu yaliyotokea , na kwamba watu wengi sana wamepitia maafa, na kwamba maisha yamejaa matatizo. Tunawakumbusha kuhusu umuhimu wa elimu na tunawapa masharti :hakuna kwenda nje masaa ya jioni au kufanya tabia mbaya na rafiki zao.

Ni familia 1,000 kote nchini zilizojisajili kama wazazi walezi wa watoto wasio na familia , kwa hiyo kuna haja ya dharura ya kuwapata wazazi walezi zaidi . Wito unatolewa kupitia viongozi wa kijamii, wafanyakazi wa jamii, kwenye mikutano ya miji na kwenye matangazo ya radio watu wajitolee kuwalea watoto wa aina hiyo.

  • Watoto wachanga wanaoachwa mpakani

Wakati Henriette na Jean-Philippe walipojisajili kwa mara ya kwanza mwaka jana kuwa wazazi walezi wa yatima kijiji cha shirika la kibinadamu la SOS liliwapa mafunzo kuhusu haki za watoto na majukumu ya kuwalea.

Haki miliki ya picha
JACK LOSH

Image caption

Kambi ya wakimbizi wa ndani katika eneo la Kaga-Bandoro, mashariki mwa Bossangoa Katika Jamuhuri ya Afrika ya kati

Halafu, walipowachukua Guy na Nelson , shirika hilo liliwatumia mwanasaikolojia kuzungumza na wavulana hao . Kama ilivyo kwa walezi wengine , Henriette na Jean-Philippe walisaini mkataba na watatembelewa bila kufahamishwa ili kuhakikisha wavulana hao wanatunzwa ipasavyo.

Kwa Guy na Nelson huenda fursa hiyo wameipata

Lakini uchungu wa maisha waliyoyapitia unaonekana katika nyuso za wavulana hao . Guy,ambaye ndiye mwenye umri mdogo, mara nyingi huonekana mwenye mawaza mengi na huzuni ,huku Nelson akionekana kuwa mwenye hasira za mara kwa mara.

Wote huwa na ndoto za kutisha mara kwa mara . “Hatutaki kurudi tena ,” anasema Guy, huku akitizama ardhini. Chini ya uangalizi wa Henriette na Jean-Philippe , wanaanza kuangalia maisha yao yajayo. Guy anataka kuwa fundi wa magari huku Nelson akitaka sana kurejea shuleni kumaliza masomo yake.

“Mara kwa mara huwa ninamuona marehemu baba yangu ndotoni ,” anasema Nelson. “Huwa ananiambia nirudi shuleni katika kijiji chetu . Hapa ni nyumbani kwetu sasa. Lazima tuanze maisha mapya.

Unaweza pia kutazama:

Wazazi waliyo na watoto walemavu Zanzibar washauriwa kutowaficha majumbaniSource link