Madam Rita ajibu malalamiko ya kijana Hamisi kutolewa kwenye mashindano ya BSS

0
14


Usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 18, 2019 wafuatiliaji wa kipindi cha Bongo Stars Search wamechukizwa na kitendo cha mshiriki wa shindano hilo, Hamisi kutolewa kwenye kinyang’aro hicho.

Madam Rita amesema kuwa  kijana huyo, Bado yupo ila kasimamishwa kutokana na ishu za masomo na ataendelea kushiriki.

Yupo sana tu he had to go do his exams za form four but yupo kambini,” Ameeleza Madam Rita kuwatuliza watazamaji wa shindano hilo.

Jana Hamisi alishindwa kuingia kwenye Top 20 ya washiriki ambao wameingia kambini na kujikuta akitolewa kwenye mashindano hayo, Huku majaji wakieleza kuwa endapo watazamaji wangependa kumuona Hamisi au washiriki wengine waliotolewa kwenye Top 10 watahitajika kumpigia kura mshiriki huyo au hao.

Washiriki wawili waliotolewa kwenye mashindano hayo, Watapata nafasi ya upendeleo kuingia kwenye fainali yaani Top 10 kwa kupigiwa kura.Source link