Kigogo serikalini atangaza makundi yote WhatsApp yafutwe

0
28


Katika kukabiliana na vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani ya darasa la saba Wilayani Chemba mkoani Dodoma, Makundi yote ya  WhatsApp ya Waratibu elimu msingi wilayani humo yamefutwa rasmi ili kudhibiti vitendo hivyo vya udanganyifu.

Akiongea leo Jumanne Septemba 10, 2019 na gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo (DED), Dkt. Semistatus Mashimba amesema hatua hiyo imechukuliwa kuepuka mathara ya kufutiwa matokeo.

Mwaka jana 2018, Matokeo ya darasa la 7 Wilayani humo yalifutwa kwa tuhuma za udanganyifu.

Wakati akingaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Charles Msonde alisema shule hizo ni shule zote zilizopo wilaya za Chemba na baadhi ya shule za wilaya ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo.

Dkt. Msonde alisema Waratibu Elimu kata kushirikiana na Wakuu wa Shule wilayani Chemba mkoani Dodoma walifungua hadi makundi ya WhatsApp ili waweze kuwasaidia wanafunzi wao kufaulu.Source link