Instagram waanza rasmi kuondoa ‘Likes’ nchini Marekani, Kim Kardashian aunga mkono ‘Nicki Minaj atangaza kujitoa’

0
13


Mtandao wa Instagram wiki hii umeanza rasmi kuondoa ‘Likes’ kwenye posts za watumiaji wa mtandao huo nchini Marekani, Jambo ambalo limesababisha baadhi ya mastaa kutoa maoni tofauti tofauti kuhusu mabadiliko hayo.

Mwanamitindo Kim Kardashian yeye amesema ni hatua nzuri kwani itapunguza chuki baina ya watumiaji na itaimarisha mahusiano yao.

Kwa upande mwingine, Rapper Nicki Minaj yeye kupitia Twitter amesema atajitoa kwa muda kwenye mtandao huo kwani hautamfanya ajisikie sawa kwa kuanza maisha mapya.

Instagram walitangaza ujio wa mabadiliko hayo Ijumaa iliyopita kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Adam Mosseri.

Marekani inakuwa ni nchi ya 8 kupata mabadiliko hayo, Baada ya nchi za Australia, Ireland, Canada na nyinginezo kufanyiwa mabadiliko hayo.Source link