Haya ndio maneno aliyoyaongea Drake, aliposimamisha Show yake Ufaransa, akitoa pole kwa taifa la New Zealand kwa janga la watu kuuawa msikitini (+ Video)

0
92


Aubrey Drake Graham alimaarufu Drake ni mmoja wa watu wengi walioguswa na tukio la kigaidi lililotokea nchini New Zealand. la kuuawa watu takribani 49 katika misikiti miwili nchini humo.
Wikendi iliyopita Drake  alisimamisha Show yake ya jijini Paris,Ufaransa ili kutoa Salam za pole kwa wahanga wa tukio hilo.

Baada ya kusimamisha show hiyo Drake aliongea maneno haya
“Nataka uelewe, kwamba sisi tukiwa na furaha hapa kuna mambo mabaya yanayotokea ulimwenguni, tunaweza bado kuungana nao kwa ajili ya kutoa poleusiku wa leo na kuona kitu kizuri kwa sababu sisi wote ni binadamu na tuko kwa ajili ya jamii zote, maeneo yote, dini zote na kuangalia, sisi tuko hapa kuonyesha upendo usiku wa leo. ” Aliendelea kusema: “Nataka kutuma upendo wangu kwa familia zote zilizoathiriwa tunakuombea na kuenea upendo zaidi kama huu ulimwenguni kote Paris, ninajivunia ninyi nyote usiku huu. . “

Ikumbukwe wiki iliyopita mtu mmoja alijirekodi akishambulia msikiti na kuua watu 49 nchini New Zealand huku akirusha Live kwenye mtandao wa Facebook, Hata hivyo mtu huyo tayari ameshakamatwa.

By Ally Juma.Source link