Fatuma Maliki: ‘Wengi hawakutarajia niwe mwanasayansi’

0
47


Haki miliki ya picha
Fatuma Maliki

Image caption

Mwanasayansi wa maabara, Fatuma Maliki

Fatuma Maliki ameugua kwa miaka 10 matatizo ya kiakili lakini ameweza kuyashinda matatizo hayo kwa kuwa mwasayansi wa maabara.

Amesimulia BBC safari ya maisha yake ambayo anasema haikuwa rahisi kwake.

Niligundua nilikuwa na tatizo fulani nikiwa na umri wa miaka 16 lakini sikuwa na uamuzi wowote kwani nilikuwa chini ya wazazi wangu.

Mambo mengi yalitokea na nilipokuwa na miaka 18 ndipo nilipofikishwa hospitalini hapo ndipo tatizo langu halisi likabainika.

Wakati nilipokutwa na hili tatizo nililazwa sana hospitalini wakidhani nina ugonjwa wa malaria ya kichwani na mwishowe wazazi wangu wakaja wakanitoa hospitalini kwamba nilikuwa na shida nyingine tofauti.

Nilitibiwa na dawa za malaria lakini sikupona, ikabidi nitibiwe kidini zaidi lakini tiba hiyo haikufaulu pia.

Lakini moyoni nilikuwa na matamanio ya kwenda shule na baadaye nilipopata nafuu mzazi wangu alikubali nirudi shuleni.

Hapo ndipo nilipoanza kuugua kila siku na maisha yangu yakawa magumu zaidi.

Nilirejea katika matibabu kwa mara ya pili nikiwa na matumaini.

Haki miliki ya picha
Fatuma Maliki

Image caption

Fatuma Maliki

Mimi nilikuwa napenda kusoma vitabu na kutizama filamu sana hasa za akili zilikuwa miongoni mwao.

Kwa wakati huo babangu alikuwa na matatizo ya kibiashara na watu wengi walimfahamu babangu kama mtu mwenye uwezo. Biashara yake ilipopata matatizo na mimi nikiugua, watu wakasema babangu ananitoa kafara. Wakati huo nilikuwa katika shule ya sekondari.

  • Google kufuta moja kwa moja matukio yanayofuatiliwa
  • R. Kelly ashindwa kesi kwa kutohudhuria mahakamani

Nilipokuwa shuleni baada ya wanafunzi wenzangu walinielewa na walinipa ushirikiano na walisaidia darasani na nikafanikiwa sana.

Dalili za tatizo langu la kiakili hunipata iwapo niko peke yangu lakini nikijumuika na watu mimi huwa kama mtu yeyote yule wa kawaida.

Licha ya matatizo hayo yote nilitafuta sababu za kuishi na pia kumpatia nguvu babangu kwa kunihangaikia na hata kunipeleka shule za gharama ya juu.

Kwa hivyo nilikuwa nahijtaji kumlipa na sikutaka akate tamaa, kwamba mtu wa maana maishani.

Image caption

Ishara ya mtu mwenye Schizophrenia

Nikuwa na ndoto ya kuwa daktari licha ya kuugua.

Nilitia bidii na sasa mimi ni mwasayansi wa maabara, na bado naendelea kukua na kujiendeleza.

Kulingana na shirika la afya duniani WHO hali hii ya matatizo ya akili huwaathiri zaidi ya watu milioni 23 kote ulimwenguni lakini ni ugonjwa nadra ikilinganishwa na matatizo mengine ya kiakili.

Vichochezi Vya Schizophrenia

  • Msongo wa mawazo
  • Urithi
  • Kasoro za kimaumbile kwenye ubongo
  • Ukosefu wa kinga mwilini na maambukizi ya magonjwa.Source link