Europa League: Chelsea yaikamua Arsenal na kushinda kombe la ligi ya Europa

0
69


Eden Hazard alifunga magoli mawili huku Chelsea ikiicharaza Arsenal katika fainali ya kombe la Europa

Eden Hazard alifunga magoli mawili huku Chelsea ikiicharaza Arsenal katika fainali ya kombe la Europa na kumpatia kocha Maurizio Sarri kombe lake la kwanza tangu achukue ukufunzi wa timu hiyo.

Olivier Giroud aliifungia Chelsea goli la kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani kupitia kichwa kizuri huku Pedro akifunga goli la pili kupitia krosi ya Hazard.

Baada ya kutoa pasi ya bao la pili , raia huyo wa Ubelgiji alifunga penalti na kufanya mambo kuwa 3-0.

Alex Iwobi aliipatia Arsenal bao la kufutia machozi mda mchache baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada lakini Hazard alifunga krosi nzuri ya Giroud na kufanya mambo kuwa 4-1.Source link