Brunei yatekeleza hukumu ya kuua kwa mawe chini ya sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

0
59


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mapenzi ya jinsia moja tayari yalikuwa ni kinyume cha sheria nchini Brunei

Nchi ndogo sana iliyopo kusini mashariki mwa bara la Asia Brunei imeanzisha sheria mpya kali za Kiislamu zinazoyafanya mapenzi ya jinsia moja kuwa kosa linaloadhibiwa kwa muhusika kupigwa mawe hadi kufa.

Sheria hizo mpya ambazo zinaanza kutekelezwa Jumatano, pia zinajumuisha uhalifu mwingine ikiwemo kuadhibiwa kwa kukatwa mikono kwa kosa la wizi.

Hatua hiyo iimeibua lawama nyingi za kimataifa.

katika hotuba yake kwa umma Jumatano , sultani wa nchi hiyo alitoa wito wa mafunzo “imara ” ya kiislamu.

“Ninataka kuona mafunzo ya kiislamu katika nchi hii yakiwa thabiti ,” Sultan Hassanal Bolkiah alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, bila kutaja sheria mpya.

Chini ya sheria mpya, watu binafsi watakuwa na hatia kufany amapenzi ya jinsia moja iwapo tu watakiri au wataonekana waki wakifanya tendo na mashahidi wanne.Under the new law, individuals will only be convicted of gay sex if they confess or are seen committing the act by four witnesses.

Mapenzi ya jinsia moja tayari yalikuwa ni kinyume cha sheria nchini Brunei na kulikuwa na hukumu yamiaka hadi 10 jela kwa mtu aliyepatikana na hatia.

Jamii ya wapenzi wa jinsia moja nchini Brunei imesema imeshituka na kuwa na hofu kutokana na “adhabu ya ukatili “.

” Unaamka na kubaini kuwa jirani zako, familia au hata yule mdada mzuri anayeuza vitafunio kando ya barabara hadhani kuwa wewe ni binadamu , au anaona ni sawa tu kuua kwa kupiga mawe ,” alisema mmoja wa wapenzi wa jinsia moja wa Brunei ambaye hakutaka kutambuliwa , alipozungumza na BBC.

Brunei, ambayo iko katika kisiwa cha Borneo, inaongozwa na Sultan Hassanal na imetajirika kutokana na mauzo ya nje ya mafuta na gesi.

Sultani huyo mwenye umri wa miaka 72-anaongoiza shirika la uwekezaji la Brunei ambalo linamiliki baadhi ya hoteli maarufu zaidi duniani ikiwemo Dorchester iliyopo mjini London na Beverly Hills Hotel mjini Los Angeles miongoni mwa nyingine.

Wiki hii mchezaji filamu wa Hollywood George Clooney na watu wengine maarufu walitoa wito wa kususiwa kwa hoteli hizo za kifahari . Mtangazaji maarufu wa TV Ellen DeGeneres pia alitoa wito kwa watu “kuamka”, akisema “tunahitaji kuchukua hatua sasa”.

Wanafunzi katika shule ya Oriental and African studies katika Chuo Kikuu cha London pia wametoa wito jengo lililopewa jina lake libadilishwe.

Watawala wa Brunei wana mali nyingi binafsi na ni watu wa jamii ya Malasyia wanaopata sehemu kubwa ya utajiri wa taifa na bila malipo ya kodi.

Theluthi mbili ya watu wa Brunei 420,000 ni waislamu.

Brunei imeendelea kuwa na sheria ya hukumu ya kifo lakini haijatekeleza hukumu ya kuua tangu mwaka 1957.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Sharia ya kiislamu ndio muongozo wa maisha ya Waislamu

Je ni mara ya kwanza kwa sheria ya kiislamu kuanzishwa Brunei?

Nchi hiyo ilianzisha matumizi ya sharia mwaka 2014 licha ya kulalamikiwa sana , na kuifanya nchi kuwa na mfumo wa sheria mbili -Sharia na ule wa kiingeleza wa Common Law. Sultani alisema wakati huo kwamba kanuni za sheria hizo zitaanza kutekelezwa kikamilifu kwa miaka kadhaa.

Awamu ya kwanza, ambayo ilihusu uhalifu unaoadhibiwa kwa kifungo cha gerezani na faini ilianza kutekelezwa mwaka 2014. Brunei ilikuwa imechelewa kuanzisha awamu mbili za mwisho, ambazo zinahusu uhalifu unaoadhibiwa kwa kukatwa viungo kwa kupigwa mawe.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Sultan Hassanal Bolkiah, ambaye pia ni waziri mkuu wa Brunei, ni miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani

Jumamosi serikali ilitoa taarifa kwenye tovuti yake ikisema kanuni za Sharia zitatekelezwa kikamilifu kuanzia Jumatano.

tangu kutolewa kwa tangazo hilo kumekuwa na malalamiko makubwa kimataifa na miito ya kuitaka nchi hiyo kuondoa sheria hizo.

“Vipengele hivi vya sheria vilip[ingwa wakati mipango ilipokuwa kwanza inajadiliwa miaka mitano iliyopita,” alisema achel Chhoa-Howard, mtafiti wa Brunei katika shirika la haki za binadamu la Amnesty International.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

George Clooney alisema sheria mpya ni ”ukiukaji wa haki za binadamu”

“Kanuni za sheria za Brunei’ ni sehemu kubwa ya sheria za nchi hiyo zikiwa na vipengele kadhaa vinavyokiuka haki za binadamu .”

Umoja wa Mataifa uliunga mkono kauli kauli hiyo ukiitaja sheria hiyo kama “katili, isiyo ya kibinadamu , na yenye kushusha hadhi ya ubinadamu”, akisema inarudisha nyuma juhudi za kulinda haki za binadamu.Source link