Boris Johnson kuwa Waziri Mkuu mpya Uingereza

0
11


Boris JohnsonHaki miliki ya picha
Reuters

Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Conservative katika kura iliyopigwa na wanachama na atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Amemshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656.

Meya huyo wa zamani wa mji wa Londona anapokea wadhifa huo kutoka kwa Theresa May kesho Jumatano.

Katika hotuba yake baada ya ushindi huo, Johnson ameahidi kuwa “ataiwasilisha Brexit, kuiunganisha nchi na kumshinda Jeremy Corbyn”.

Akizungumza mjini London, alisema: “Tutaipa nchi nguvu.

“Tutaiwasilisha Brexit kufikia Oktoba 31 na kuchukua fursa zote zitakazotokana na muamko mpya wa inawezekana.

“Tutajiamini upya na tutainuka upya na kuondosha shaka na fikra za kutojiamini.”

Bi May amempongeza Johnson, na kumauhidi “ushirikiano wake kikamilifu kutoka nafasi ya nyuma”.

Rais wa Marekani Donald Trump pia ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akimpongeza Johnson, na kuongeza: “Atakuwa mzuri mno!”

Takriban wanachama 160,000 wa Conservative walikuwa na fursa ya kupiga kura na katika waliojitokeza ni 87.4%.

Asilimia ya kura kwa Johnson – 66.4% – ilikuwa chini ya aliyojishindia waziri mkuu wa zamani David Cameron mnamo mwaka 2005 aliyejinyakulia 67.6%.Source link